SERIKALI YAMPA MKANDARASI MIEZI MITATU UJENZI WA DARAJA LA LUKULEDI NACHINGWEA
#KAZIINAONGEA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Ujenzi, imetoa miezi mitatu kwa Mkandarasi M/s China Railway 15 Bureau Group Cooperation anayejenga Barabara ya Nachingwea-Ruangwa-Nanganga (KM 106), kukamilisha ujenzi wa daraja la Lukuledi.
Agizo hilo limetolewa Januari 11, 2025 na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega wakati akikagua ujenzi wa Barabara ya Nachingwea-Ruangwa-Nanganga yenye urefu wa Kilometa 106, na madaraja na kusisitiza kuwa, fedha zipo hivyo ni wajibu wa mkandarasi kuongeza kasi ili wakazi Ruangwa na Nachingwea wanufaike na mradi huo.
"Mtendaji Mkuu wa TANROADS simamieni mradi huu ukamilike kwa wakati na ujengwe kwa ubora ili udumu kwa muda na kuwawezesha wananchi wa Wilaya za Ruangwa na Nachingwea kunufaika kwa kuyafikia masoko ya mazao yao kwa urahisi," amesisitiza.
Amesema ujenzi wa barabara hiyo uendane na uwekaji taa za barabarani ili kuondoa giza na kuchochea ukuaji wa Miji na hivyo kuwawezesha wananchi kufanya biashara muda wote.
#KAZIINAONGEA
0 Comments