SERIKALI YAMTAKA MKANDARASI CHANZO CHA MAJI MTO NYANGAO, KUKAMILISHA KAZI NDANI YA MIEZI MIWILI


SERIKALI YAMTAKA MKANDARASI CHANZO CHA MAJI MTO NYANGAO, KUKAMILISHA KAZI NDANI YA MIEZI MIWILI

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Maji, imemtaka Mkandarasi STC CO LTD anaejenga chanzo cha maji katika Mto Nyangao -Chiuwe Wilayani Lindi, kukamilisha kazi ndani ya miezi miwili.

Akitoa maagizo hayo, wakati wa ziara yake Wilayani Lindi kwenye Mradi wa maji Nyangao- Mtama na mradi mkubwa wa vijiji 56 kwa kutumia chanzo hicho cha Mto Nyangao/Chiuwe Lindi kwenda Wilaya za Ruangwa na Nachingwea, Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Methew amesema kuwa, Mkandarasi anapaswa kukamilisha kazi hiyo kwa wakati ili kuwaondolea wananchi adha ya maji, na kwamba mradi huo umegharimu takribani Shilingi Bilioni 119.

Baada ya kukagua ametumia nafasi hiyo kuagiza kuwa, hadi kufikia mwezi Machi,2025, Wananchi wa Mtama na Nyangao waanze kupata huduma ya maji kupitia mradi wao mpya ambao unatekelezwa na Mkandarasi Halem Co Ltd.

Pia amewataka Meneja wa RUWASA Mkoa na Meneja wa Wilaya kukaa na Mkandarasi Halem Co Ltd kwa ajili ya kufanya majadiliano kwa kazi inayoongezeka ili kazi hiyo ifanyike ndani ya mwezi mmoja

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva amesema, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameidhinisha fedha nyingi za miradi ya maji Wilayani humo kiasi cha Shilingi 4.577 Billion na Mradi wa kutoka Lindi kwenda Ruangwa na Nachingwea kwa 119.1Billion, naye jukumu lake ni kusimamia na kuhakikisha miradi inajengwa kwa ubora ili idumu vizazi na vizazi na kuondoa kabisa adha ya maji kwa kumtua mama ndoo kichwani.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments