#KAZIINAONGEA
Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini, (Ruwasa), imefanikiwa kuchimba jumla ya visima tisa (9) kati ya 10 vya maji safi na salama Wilayani Lindi, kwa gharama ya ya Shilingi Milioni 600 ikiwa ni utekelezaji wa programu ya uchimbaji visima 900 kwa nchi nzima.
Programu hiyo inalenga kuhakikisha zaidi ya asilimia 85 ya wananchi wa maeneo ya vijijini wanapata huduma ya maji safi na kutimiza adhma ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani.
Kaimu Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Lindi Mhandisi Athanas Lume Patrick amesema, visima vinne kati ya hivyo vimechimbwa katika Jimbo la Mchinga vitakavyohudumia wakazi 2,604 huku visima vitano vimechimbwa kwa Halmashauri ya Mtama vitawahudumia takribani wakazi 4,709 na hivyo kuongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kutoka 76 hadi 82.4
Ametaja maeneo ambayo vimechimbwa kuwa ni pamoja na Dimba, Ruchemi, Kitongoji cha Runyu, Makangala, Kitongoji cha Likonde kwa upande wa jimbo la Mchinga wakati jimbo la Mtama vikichimbwa katika maeneo ya Vijiji vya Utimbe, Madingo, Milamba, Litingi na Kitongoji cha Mbindo (Nahukahuka A).
Baadhi ya wananchi kutoka katika kijiji cha Dimba kata ya Kilolambwani akiwemo Saidi Abdalah, Mwenyekiti wa Kijiji hicho na Desteria Joseph Chilumba wamelalamikia kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji kwenye vyanzo vya asili ambavyo wamedai wanashirikiana na wanyama kama Tumbili na kwamba uchimbaji wa visima hivyo unakwenda kuondoa adha hiyo.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments