SERIKALI YATAKA TAASISI ZA DINI KUDUMISHA AMANI


SERIKALI YATAKA TAASISI ZA DINI KUDUMISHA AMANI

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Rais Samia Suluhi Hassan, imezitaka taasisi za dini nchini kuhubiri amani kwa waumini wao ili nchi iendelee kuwa salama.

Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Januari 14,1025, alipokutana na viongozi wapya wa Kitaifa wa Jumuiya ya Kiislam ya Ahmadiyya ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amezitaka taasisi za dini nchini kuendelea kuwahamasisha waumini wake kudumisha amani na kushiriki katika shughuli za maendeleo.

 Viongozi hao wapya wa jumuiya hiyo walikwenda kwa ajili ya kijitambulisha kwa Waziri Mkuu.

"Fanyeni kazi kwa uhuru na wala msiwe na mashaka. Wahamasisheni Watanzania washiriki katika shughuli za kimaendeleo."

Pia amewashauri viongozi hao wabuni miradi ya kiuchumi kwani Tanzania kuna fursa nyingi za kimaendeleo.

Aidha Majaliwa ameipongeza jumuiya hiyo kwa uwekezaji ilioufanya katika sekta mbalimbali zikiwemo afya na elimu ambapo ameahidi kuwa Serikali itaendelea kuwapa ushirikiano katika jitihada zao hizo.

Amesema Serikali kwa upande wake inathamini na kutambua mchango mkubwa unaofanywa na taasisi za dini.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments