SHIRIKISHO LA WALIMU KANDA YA ZIWA WAJIVUNIA MAENDELEO YA MRADI WA BWAWA LA KUFUA UMEME JNHPP


SHIRIKISHO LA WALIMU KANDA YA ZIWA WAJIVUNIA MAENDELEO YA MRADI WA BWAWA LA KUFUA UMEME JNHPP

Shirikisho la walimu kutoka Mikoa ya  kanda ya ziwa leo wamefanya ziara katika mradi wa Bwawa la kufua Umeme la Julius Nyerere na kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wake ambao umefikia asilimia 99.55 unaotarajia kuwa namchango mkubwa kwa maendeleo ya wananchi kiuchumi na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kutembelea Bwawa hilo Msaidizi wa Rais katika masuala ya siasa Benedict Kikove ambaye ameambata na  walimu hao amesema kukamilika kwa mradi huo utaenda kuondoa kabisa changamoto za upatikanaji wa Umeme nchini.

"Hawa walimu wamesafiri umbali mrefu kujionea wenyewe mradi huu ambao sehemu kubwa ya utekelezaji wake umekamilka kwa asilimia 100 kikubwa ni kujifunza maendeleo ya kimkakati na kuwaeleza wanafunzi mambo yanayofanywa na Serikali katika nchi yao" Alisema Benedict.


Nae Mratibu wa Mradi Mhandisi John Skauki amesema kauli ya Mheshimiwa Rais kwamba atausimia mradi huu kwa vitendo imewapa nguvu ya kufanya kazi kwa kasi na anaimani utatakamilika kwa wakati.

"Sisi tumepata nguvu na ujasiri baada ya Serikali kuweka nia ya dhati kabisa hasa baada ya kauli ya Mheshimiwa Rais kwamba atasimamia miradi ambayo aliahidi kuitimiza na kuikamilisha kwa vitendo tunamshukuru" Alisema Mhandisi Skauki.


Nao baadhi ya walimu kupitia shirikisho hilo wamesema wamejionea thamani halisi ya Fedha ambazo zimetumika katika utekelezaji wa mradi hivyo endepo mradi huo utakamilkka rasmi tatizo la Umeme nchini Tanzania litabaki kuwa ni historia hivyo kazi yao sasa ni kushirikiana na Serikali kuilinda miundombinu na mazingira ili kurithisha kizazi cha sasa na kijacho.

"Tumeelezwa kuwa mradi huu ni wa zaidi ya shilingi Trilioni 6 ambapo mpaka sasa hivi Serikali ya awamu ya sita imeshalipa zaidi ya asilimia 95 kwa jambo hilo peke yake nchi itapaa kiuchumi"Alisema Dominick Haule

Post a Comment

0 Comments