SILINDE AIPONGEZA TPHPA NA KUAGIZA UJENZI WA MAABARA ZA KISASA VITUO VYA UKAGUZI RUSUMO NA MUTUKULA



SILINDE AIPONGEZA TPHPA NA KUAGIZA UJENZI WA MAABARA ZA KISASA VITUO VYA UKAGUZI RUSUMO NA MUTUKULA

Ujenzi wa vituo hivyo unafanywa ili kuboresha huduma na utendaji wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) hii ni hatua kubwa kwa Tanzania, kwani inaonesha dhamira ya Serikali kuboresha mifumo ya ukaguzi wa mazao na kuhakikisha usalama wa afya ya mimea na viuatilifu katika biashara ya Kimataifa.

Mwandishi wetu, Kagera

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) ameipongeza Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA) kwakusogeza huduma mipakani ambapo ameiagiza kujenga maabara za kisasa katika vituo vya ukaguzi vya mpaka wa Rusumo Ngara (karibu na nchi ya Rwanda) na Mutukula (karibu na nchi ya Uganda) ifikapo Februari 2025 ili kuboresha utendaji kazi wa taasisi hiyo. 


Kauli hiyo ameitoa wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya ukaguzi vya TPHPA wa vituo hivyo katika Mpaka wa Rusumo Ngara na Mutukula iliyopo Wilaya ya Missenyi katika mkoa wa Kagera.

"Maabala hizi zikijengwa zitasogeza huduma na kuboresha utendaji kazi wa taasisi hii muhimu na kurahisisha zaidi utendaji kazi wa vituo hivyo ambavyo vinaenda kutoa majibu sahihi kwa wakulima wetu nchini" amesema Silinde

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA), Prof. Joseph Nduguru amesema kuwa atatekeleza agizo.

Amesema kuwa TPHPA watahakikisha kuwa vituo hivyo vinajengwa maabala ya kisasa zitakazo kidhi mahitaji ili kuboresha utaoji wa huduma. 

“Mpaka wa Rusumo na Mutukula ni muhimu sana katika biashara ya mazao ya kilimo, na kupitia ujenzi wa maabara za kisasa, tunaamini tutaongeza tija na kuhakikisha kuwa mazao yanayohitaji kusafirishwa nje ya nchi yanakaguliwa kwa ufanisi zaidi” 

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TPHPA Kanda ya Ziwa, Mary Leina, ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024, vituo vya Rusumo na Mutukula vilifanya kazi nzuri kwa kukagua mazao yenye uzito wa tani 331,537. 

TPHPA ilikusanya zaidi ya shilingi milioni 374 kutokana na huduma za ukaguzi, na sehemu kubwa ya mazao hayo yalisafirishwa kwenda nchi za nje, hasa Mchele, Mtama, Maharage, na Molasses.

Kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025, Mpaka wa Rusumo tayari umehakiki tani 98,275.67 za mazao, na kuingiza fedha zaidi ya shilingi milioni 140, huku Mpaka wa Mutukula ukikagua tani 51,692.003 za mazao na kupata zaidi ya cha shilingi milioni 101.


Post a Comment

0 Comments