STOF YATATUA CHANGAMOTO YA MAJI KATIKA SHULE TATU SONGEA
Mwandishi wetu, Ruvuma
TAASISI ya Isiyokuwa ya Kiserikali ya St.Teresa Orphans Foundation (STOF) imetoa Zaidi ya shilingi milioni 30 kukarabati majengo ,kununua madawati 25,kukarabati na kuchimba visima vitatu katika shule za msingi tatu Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.
Hayo yamesema na Mkurugenzi wa STOF nchini Tanzania Moses Nyirenda katika hafla ya kuishukuru STOF iliyofanyika katika shule ya msingi Unangwa ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mkurugenzi wa STOF nchini Marekani Teresa Nyirenda.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa STOF nchini Tanzania,kati ya fedha hizo,jumla ya shilingi milioni 15 zimetolewa kwa ajili ya kukarabati majengo ya shule ya msingi Unangwa, shilingi 700,000 zimetumika kununua madawati 25 katika shule hiyo na shilingi 600,000 zimetumika kukarabati kisima cha maji.
Nyirenda amebainisha Zaidi kuwa STOF pia imetoa shilingi milioni 15.9 kuchimba visima viwili vya maji katika shule za msingi Msamala na Mkuzo hivyo kutatua changamoto ya ukosefu wa maji kwa wanafunzi katika shule hizo na kuzuia magonjwa mbaimbali ikiwemo ugonjwa wa matumbo.
Akizungumza mara baada ya kukagua miradi katika shule tatu za Unangwa,Msamala na Mkuzo,Mkurugenzi wa STOF nchini Marekani Teresa Nyirenda amewapongeza walimu na Kamati za Ujenzi kwa kusimamia vema utekelezaji wa miradi hiyo iliyofanikisha kupeleka maji katika shule tatu za msingi hivyo kutatua changamoto ya maji kwa wanafunzi katika shule hiyo.
“Unapoona mtoto hajakunywa maji tangu asubuhi,halafu chooni hakuna maji ni kitu ambacho kimenishitua hivyo sio STOF tu bali inatakiwa kuhamasisha hata wadau wengine kupita katika shule za msingi na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo ikiwemo ukosefu wa maji nimejifunza kitu kikubwa sana kupitia ziara hii’’ Nyirenda,alisisitiza.
Ameahidi kuendelea kusaidia changamoto nyingine zikiwemo ukarabati wa vyoo vya wanafunzi katika shule ya msingi Unangwa ambapo amewapongeza Kamati ya ujenzi kwa kutumia fedha vizuri za kukarabati majengo ya shule hiyo ambayo yalikuwa chakavu.
Amesema Taasisi binafsi zinawajibu wa kuisaidia serikali katika kuhakikisha huduma muhimu zinawafikia wananchi kwa kuwa serikali pekee inasimamia miradi mingi
0 Comments