TANZANIA NA COMORO KUSHIRIKIANA SEKTA YA NISHATI
#KAZIINAONGEA
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imebaliana na Serikali ya Comoro maeneo kadhaa ya ushirikiano katika Sekta ya Nishati.
Makubaliano hayo yamefanyika hivi karibuni wakati
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Mashaka Biteko alipokutana na Waziri wa Nishati wa Umoja wa Visiwa vya Comoros, Dkt Aboubacar Anli na kukubaliana maeneo kadhaa ya ushirikiano katika Sekta ya Nishati.
Awali, Waziri wa Nishati wa Comoros ameeleza umuhimu wa ushirikiano kwenye sekta hiyo baina ya Comoro na Tanzania hususan kuanza mazungumzo kwa ngazi ya wataalam ili kufanya upembuzi wa maeneo muhimu ya kuanzia hususan katika uzalishaji na usambazaji umeme kwenye visiwa hivyo akieleza pia azma ya Serikali yao kuzalisha umeme kwa vyanzo vya nishati ya mvuke (Geo Thermal) inayopatikana kwa wingi visiswani humo.
Aidha, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa maandalizi mazuri na mkutano wa mafanikio wa Wakuu wa Nchi kuhusu Nishati uliomalizika hivi karibuni.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Mkuu Dkt.Biteko ameeleza utayari wa Tanzania katika kushirikiana na Comoro kwenye maeneo tajwa na kuelekeza taratibu rasmi ili kuweza kufikiwa makubaliano rasmi kwenye Sekta ya Nishati na uwezo na uzoefu wa Tanzania katika eneo hilo.
TANZANIA NA COMORO KUSHIRIKIANA SEKTA YA NISHATIMazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Khatib Kazungu, Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta za Nishati na Maji, Bwana Andililo Tagalole, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Boniface Nyamohanga Gisima, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania Bi Rosemary Jairo na Balozi wa Comoro Nchini Tanzania Dkt Ahamada El Badaoui.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments