TANZANIA YANADI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU UAE.


TANZANIA YANADI MIRADI YA NISHATI JADIDIFU  UAE. 

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kupitia Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu Januari 11, 2025 imeshiriki Mkutano wa 15 wa Baraza la Kimataifa la Wakala wa Nishati Jadidifu IRENA mjini Abu Dhabi, Falme za Kiarabu.

Katika Mkutano huo Dkt. Kazungu ameelezea juu ya miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia vyanzo vya nishati jadidifu inavyozingatia utunzaji wa mazingira, na kuinua uchumi wa nchi.

 Dkt. Kazungu amesema miradi ya kuzalisha umeme kwa kutumia nishati jadidifu inayotekelezwa nchini Tanzania inazingatia umuhimu wa utunzaji wa mazingira na ushirikishwaji wa wananchi kwenye maeneo yanayozunguka miradi hiyo, Dkt Kazungu ameyasema hayo wakati wa mjadala wa wazi kujadili athari za mazingira na umuhimu wa miradi ya nishati jadidifu kwenye utunzaji wa mazingira

‘’Tanzania imekuwa ikitilia mkazo umuhimu wa miradi ya nishati jadidifu kwenye utunzaji wa mazingira na imeleta tija kubwa kiuchumi, kijamii na kimazingira’’ amesema Dkt. Kazungu 

Aidha, ametaja faida za kiuchumi za miradi ya nishati jadidifu kuwa ni pamoja na ongezeko la ajira wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo na kuinua hali ya kipato kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya miradi hiyo kwa kutolea mfano wa mradi wa Bwawa la kufua umeme la Mwalimu Julius Nyerere (JNHPP) ambapo takribani ajira 8,000 zimepatikana kupitia mradi huo. 

Vile vile, Dkt. Kazungu ameliambia baraza la IRENA kuwa kwa upande wa utekelezaii wa miradi ya nishati jadidifu kwa upande wa mazingira,imesaidia kupunguza hewa ya ukaa kwenye uso wa dunia yaani green house gases na kuifanya ikolojia kuwa nzuri na kuepusha ukame na kuongeza kuwa miradi mingine ni pamoja na ule wa Kishapu Shinyanga wa Megawati 150 pamoja na miradi ya joto ardhi iliyoko mkoani Mbeya na Songwe ya Kejo na ziwa Ngozi.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments