TARI WATOA ELIMU KWA WAKULIMA NA WAJASILIMALI KUEPUKA HASARA BAADA YA MAVUNO
Mwandishi wetu, Pwani
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) kupitia kituo cha TARI Kibaha yenye dhamana ya kufanya tafiti za kilimo nchini chini ya wizara ya kilimo imekuja na suluhisho la kuwaepusha na hasara ya zao la nyanya baada ya mavuno.
Mafunzo hayo ya uongezaji thamani katika zao la nyanya yanaenda kupunguza upotevu baada ya Mavuno ambao kwa zao hilo unakadiriwa kuwa asilimia 25-30.
Mafunzo hayo yanayoratibiwa na TARI Kibaha kwa kushirikiana na Shirika la maendeleo ya viwanda vidogo nchini (SIDO) yanayofanyika kwa siku nne Januari 14-17,2025 katika eneo la Dumila, Wilaya ya Kilosa yakijumuisha Wakulima na wajasiriamali 15.
Akifungua mafunzo hayo Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Elina dastan amewaasa washiriki kuzingatia yale wanayofundishwa ili kujiongezea tija kupitia mnyororo mzima wa thamani wa zao la nyanya.
Mafunzo haya ni matokeo ya Utekelezaji wa Mradi wa "Kupunguza Upotevu baada ya Mavuno na Kuongeza Kipato cha Wakulima Kupitia bidhaa za Nyanya", unaofadhiliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Miongoni mwa bidhaa zinazotokana na usindikaji wa nyanya ni kama vile; sosi ya nyanya (tomato sauce), uji mzito wa nyanya (tomato paste), jamu na unga wa nyanya.
0 Comments