#chaiyetufahariyetu
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Machare Estate, Madam Bente, (kushoto)akiwa na Mtaalamu kutoka Bodi ya Chai Tanzania (TBT) Godlove Elia Myinga ambaye ni Afisa Mkuu Mipango na Uhamasishaji wa TBT,( wa katikati) wakati Mtaalamu huyo alipotembelea shamba la Machare.
Bodi ya chai Tanzania TBT imetembelea Kampuni ya Machare Estate inayomiliki kiwanda cha kuchakata majani mabichi ya chai kwa ajili ya kupata chai kavu maalumu yaani orthodox tea ambacho kipo Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akiwa katika kiwanda hapo Mtaalamu kutoka Bodi ya Chai Tanzania (TBT) Godlove Elia Myinga ambaye ni Afisa Mkuu Mipango na Uhamasishaji wa TBT ametembelea Maabara ya Chai ambapo ndani yake ndipo chai inaandaliwa kwa ajili ya uonjaji baada ya kutengenezwa.
Kiwanda hicho cha chai kinatengeneza aina mbalimbali ikiwemo ambazo hazijafanyiwa uchachuaji yaani "unfermented tea" pamoja na zile ambazo zimefanyiwa uchachuaji " fermented tea'".
#chaiyetufahariyetu
0 Comments