UANDIKISHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA WAANZA LINDI
Mwandishi wetu, Lindi
Zoezi la uboreshashi wa daftar la kudumu la mpiga kwa kura Mkoa wa Lindi limeanza rasmi tarehe 28 January na Linatarajiwa kukamilika siku ya jumaatatu ya tarehe 03 February 2025 huku likitarajiwa kuandikisha na kuboresha taarifa za jumla ya wakazi 102151 wa Manispaa ya Lindi.
Aitha jumla ya vituo 274 vya uboreshashi wa daftar la kudumu la mpiga kura Manispaa ya Lindi yenye majimbo ya uchaguzi mawili ya Lindi mjini na Mchinga,Ambapo kwa Jimbo la Lindi mjini wanatarajia kuandikisha wakazi 58,483 na Mchinga wanatajia kuaandikisha na kuboresha taarifa za wakazi 43668.
Katibu tawala wa Mkoa wa Lindi bi Zuwena Omari amewaomba wanainchi wote wenyesifa kuweza kujitokeza katika kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari hilo Ili kupata sifa za kupata haki ya Msingi ya kupinga kura ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Zuwena Omari Amesema katika kipindi hiki Cha uandikishaji na uboreshashi wa daftar la kudumu la mpiga kura anawaomba wanainchi wenye sifa waweze kujitokeza katika kujiandikisha na kuboresha taarifa zao Ili waweze kupata haki zao za Msingi pindi utakapo fika wakati wa uchaguzi.
"Binafsi nimekuja kuboresha taarifa zangu za mpiga wito wangu kwa wanainchi wale ambao wamefikisha miaka 18 na hawakuweza kujiandikisha awamu iliyopita wajitokeze katika kujiandikisha na kwa wale ambao wamehama kwenye makazi yao ya awali ususani kwenye kata zao za awali,waliopoteza kadi zao na wale ambao majina yao yamebadilika"Zuwena Omari
Aitha Zuwena Omari ametoka wito kwa wanainchi wote kuweza kufanya hamasa kwa wanainchi wengine waweze kujitokeza katika zoezi hilo waende kuboresha taarifa zao wakifanya hivyo itawasaidia kwenye kushiriki haki yao ya Msingi ya kupinga kura ambayo ni haki ya Msingi na ya kidemokrasia.
Nae Mkuu wa wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva akiwa kwenye kituo Cha uboreshashi wa daftar la kudumu la mpiga kura Amesema anawaomba wakazi wa Mkoa wa Lindi pamoja na wilaya ya Lindi kuweza kujitokeza katika kuboresha daftari la hilo.
"Rai yangu kwa wanainchi wote wenye sifa za kupiga kura muweze kujitokeza katika uboreshashi wa taarifa za mpiga kura kwasababu kupiga kura ni haki ya msingi "Mwanziva
Akizungumza kwenye zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura leo Jumatano Januari 29,2025 Ofisa muandikishaji wa dafari la wapiga kura,Juma Mnwele amesema kuwa Manispaa ya Lindi wanatarajia kuandikisha wapiga kura wapya,102,151ambapo jimbo la mchinga wataandikisha wapiga kura 43,668 na jimbo la Manispaa wataandikisha wapiga kura 58,483.
Lengo la kuboresha taarifa nikwamba ,kunawengine wanaboresha taarifa zao kwa kuhama maeneo yao, kadi kupotea au majina yalikosewa,lakini kunawengine watafutwa endapo wataonekana hawana sifa,kutokana na sababu mbalimbali kama ,mtu alifariki na wengine kukana uraia wake".Amesema Mnwele.
Nae Sharifa Selemani mwenye ulemavu wa macho Amesema anawapongeza tume ya Taifa ya uchaguzi kuwapa kipaimbele watu wenye nahitaji maalumu wakati wa uboreshaji wa taarifa za mpiga kura kwa kuwapa nafasi pindi wanapo fika kwenye vituo.
"Mimi nsishukuru serikali pamoja natume kwa kutupa kipaumbele sisi wenye ulemavu nimekuja hapa sijakaa foleni wamenipisha nimeenda kujiandikisha bila hata kuchelewa"Sharifa
Ismael Thabiti mjumbe wa Amesema zoezi hilo la uboreshashi wa taarifa kwa upande wake limekua jepesi tofauti na alivyo tarajia hatakama mtu anaweza kuenda kuboresha ndani ya mda mchache taarifa zinakamilika na kuendelea na shughuli zingine.
"Nilivyo fikiria ni tofauti na nilivyo kuta hapa ni tofauti Yani hata dakika 10 hazizidi taarifa zangu zimekamilika na ninaenda kuendelea na kazi zangu,nikitoka hapa nitaenda kua balozi mzuri kwa watu wengine"
Mtanda Manispaa ya Lindi.
0 Comments