UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI KATIKA WILAYA YA NANYUMBU.



UZINDUZI WA MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA NCHINI  KATIKA WILAYA YA NANYUMBU. 

 Mahakama  ya Wilaya ya Nanyumbu Leo tarehe 27/1/2025  imefanya Matembezi ya Amani ya Kilometa tatu(3) ya kushiriki Uzinduzi wa wiki ya Sheria Yaliyoongozwa na Mgeni Rasmi  Mkuu Wa Wilaya ya Nanyumbu,  Mhe. Christopher Edward Magala  yaliyoanzia Mahakama ya Wilaya Nanyumbu  hadi katika viwanja vya Mangaka Amcos.

Kauli mbiu ya Maadhimisho yalikuwa, TANZANIA YA 2050 NAFASI YA TAASISI ZINASIMAMIA HAKI MADAI KATIKA KUFANYA MALENGO MAKUU YA DIRA YA TAIFA YA MAENDELEO.


Akizungumza  katika Uzinduzi huo, Mkuu Wa Wilaya Nanyumbu Mhe. Christopher Edward Magala alisema kuwa Mahakama ni sehemu ya Mhimili Muhimu Unaotekeleza Maendeleo ya Nchi, hivyo kupitia Matembezi ya Ufunguzi wa wiki ya Sheria, Amewataka watumishi wote wa Mahakama Kutenda haki kama ilivyo Kauli Mbiu ya Mahakama isemayo Uadilifu,welding na Uwajibikaji ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa. 

Aliwakumbusha pia  Wananchi kuwepo kwa KAMPENI YA KITAIFA YA MAMA SAMIA Ambayo kwenye Mkoa wa Mtwara ilianza tarehe 24/1/2025 hadi tarehe 2/2/2025 na katika Halmashauri ya Nanyumbu imezinduliwa Leo tarehe 27/1/2025 Mpaka tarehe 3/2/2025 na timu  ya Halmashauri inapita kwenye kata na vijiji kwa Dhumuni ya kutoa Elimu na huduma ya Sheria , Hivyo wanainchi wajitokeze katika kupata Elimu hiyo.

Post a Comment

0 Comments