WAKAZI 80,000 KUNUFAISHWA NA MIRADI YA MAJI LINDI


WAKAZI 80,000 KUNUFAISHWA NA MIRADI YA MAJI LINDI INAYOJENGWA KWA MABILIONI

Mwandishi wetu, Lindi

Zaidi ya wakazi 80,000 wa mkoa wa lindi wanatarajia kunufaika na miradi mbalimbali ikiwemo ya maji ambapo serikali imetoa zaidi ya bilioni 85 ili kukamilisha miradi hiyo ili kuhakikisha kuwa maji yanapatikan kwa asimilia 85.

Katika kipindi cha miaka 4 (Machi, 2021 hadi Disemba, 2024) Serikali imeidhinisha jumla ya kiasi cha fedha za kitanzania 5.71 Billion kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 17  jimbo la Mchinga na Shilingi 12.79 billioni kwa ajili ya ya utekelezaji wa miradi 13 katika Halmashauri ya Mtama ikiwemo miradi 5 ya uchimbaji wa visima katika kila jimbo la uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa Zaidi ya asilimia 85 ya wananchi waishio vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama.


Akiwa katika ziara ya kimkakati ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva ametembelea miradi miwili  ya uchimbaji wa visima vya maji Dimba pamoja na kitongoji cha Runyu kata ya Kitomanga.

Amesema kuwa adhima ya Dkt. Samia Suluhu ya kutoa  magari ya uchimbaji wa visima mia 900 vya maji katika kila Mkoa yanafanya kazi na visima hivyo vinachimbwa Ili wananchi waweze kurahisishiwa kupata maji yaliyo safi na Salama.

Aidha amewataka wahandisi na wasimamizi  miradi hiyo mwili kukamilisha Mradi ndani ya siku 14 Ili wanainchi hao waweze kupata maji haraka Ili waweze kuondokana na adha ya kufuata maji umbali  mrefu

Aidha wakazi 166493 wa Halmashauri ya Mtama watanufaika na mradi huo kwa halmashauri nzima na  wakazi 71,174 wa Kata 10 za  jimbo la Mchinga mchinga watanufaika na mradi huo.

"Kwenye makaratasi tumeona mnasema vimechimbwa lakini nimekuja kuona nimeona bado tumemefika hatua nzuri na tunaimani na nyinyi maombi maagizo maelekezo tunaomba kazi hii ikamilike ndani ya mwezi huu wa kwanza na mwezi wa pili tutarejea hapa kuona maji mwamwamwa"Mwanziva


Nae Kaimu Meneja wa RUWASA Athanas Lume Amesema hadi kufikia Disemba 2024 wastani wa upatikanaji ya maji safi na Salama katika Halmashauri ya Mtama imefikia asilimia 74.4  ambayo zaidi ya vijiji 60 vinapata huduma hiyo na kwa jimbo la Mchinga huduma ya hiyo imeanza kupatikana kwa asilimia 77 na vijiji 28 tayari kunufaika mradi.

Aidha Mhandisi Lume amesema kuwa lengo la uanzishwaji wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA)imwanzishwa kwa mujibu wa kifungu namba 42 Cha Sheria ya huduma ya maji na usafi wa  mazingira No 5 ya mwaka 2019 ikiwa na jukumu la kupanga, kusanifu ,na kusimamia miradi ya maji vijijini .

Nae Sofiana Thomas Mkazi wa Dimba ameishukuru serikali kukiweka Kijiji hicho kwenye mradi huo wa visima 900 kwa kua wanatembea umbali mrefu kufuata maji ambayo ni machafu na hayana sifa kwakua ni machafu sana na wanatumia pamoja na wanyama .

"Mimi nasema nashukuru serikali ya mama Samia kutuletea maji haya kwasababu maji kwetu ni changamoto tunatumia maji pamoja na wanyama yanakua machafu Hadi tuyaweke kwa mda yatengani maji na matope ndyo tutumie kwetu ni jambo la faraja Leo kuona tutapata maji hapa hapa kijijini Nashukuru sana serikali "


Nae Selemani Rutufi Amesema kipindi Cha nyuma hata ndoa zao zilikua zinayumba kutokana kutoaminiana kwasababu ya kuchelewa kurudi nyumbani kutokana na umbali mrefu.

"Tunashukuru kwakweli serikali kwa kutuletea maji ndoa zetu sasa zitapona na tutakua na uhakika wa kupata maji safi na Salama n maisha yetu yataenda kubadikika kwasababu maji ndiyo kila kitu kwenye maisha ya binadam "Selemani

Post a Comment

0 Comments