#KAZIINAONGEA
Wananchi wengi wa mkoa wa Iringa wameonesha kuguswa na uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan unaojali maslahi yao na kuamua kutoa shukurani zao kwake.
Kwa nyakati tofauti wananchi wameonyesha kufurahishwa na namna serikali ya Rais Samia ilivyowapelekea huduma za barabara, maji, shule, hospitali pamoja na kuwatengea mikopo yenye mashariti nafuu.
Hatua hiyo imemfanya Mkuu wa wilaya ya Iringa Kheri James kupita katika maono ya Rais Samia ambapo hivi karibuni amewashukuru na kuwapongeza wadau mbalimbali wilayani humo kwa kufanikisha uzinduzi wa Jukwaa la Mafanikio la wilaya ya Iringa lenye lengo la kueleza mafanikio yaliyoletwa na Rais Samia kwenye wilaya hiyo katika Sekta mbalimbali na kuongeza kasi ya uwajibikaji na uwazi kwa umma.
Kheri James ametoa Shukurani na pongezi hizo katika hafla fupi iliofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa wilaya na kuhudhuriwa na Viongozi wa Taasisi za Umma, Viongozi wa dini, Viongozi wa Kimila, Viongozi wa jumuiya mbalimbali za kijamii, Watumishi pamoja na wanahabari.
Akizungumza katika hafla hiyo Kheri James ameeleza kuwa uzinduzi wa jukwaa hilo umesaidia kuhabarisha wananchi, kuongeza uwajibikaji, kujenga umoja, kuweka uwazi na kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Aidha ameeleza kuwa kupitia uzinduzi wa Jukwaa hilo Taarifa za miradi na utendaji wa Taasisi za umma umekua wazi na Wananchi wamepata fursa ya kutembelea miradi yao na kujionea hatua za maendeleo zilizofikiwa.
Kupitia hafla hiyo amewashukuru Viongozi, Watumishi, Wananchi na Wanahabari kwa kuwezesha uzinduzi wa jukwaa hilo na kwa ushiriki wa kila mmoja katika kufanikisha lengo na tija ya kuanzishwa kwa jukwaa hilo.
Ofisi ya Mkuu wa wilaya pia ilikabidhi vyeti vya Shukurani na Pongezi kwa Taasisi na Jumuiya mbalimbali ambazo zilifanikisha uanzishwaji wa Jukwaa hilo.
Jukwaa la Mafanikio wilaya ya Iringa, litakua ni jukwaa litakalowapa fursa Wananchi wa wilaya ya Iringa kushiriki, kusikiliza na kutembelea hatua mbalimbali za maendeleo zilizofikiwa katika wilaya hiyo kupitia sekta ya Umma na binafsi.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments