WANANCHI NAMTUMBO WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUTOA MATREKTA MATATU
Mwandishi wetu, Ruvuma
Wananchi wa Wilaya ya Namtumbo wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kugawa matrekta matatu ambayo yameanza kunufaisha wakulima wa tarafa tatu za wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Mhe. Ngollo Malenya, amewataka wakulima kutumia matrekta hayo kwa ufanisi ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kimkakati kama mbaazi, ufuta, soya, na mazao mengine ya kibiashara.
Kwa upande wake Said Libaba, mkulima kutoka kitongoji cha Suluti, amepongeza mpango huo wa serikali ya awamu ya sita, akisema matrekta hayo yameleta mabadiliko chanya kwa wakulima wa Namtumbo.
0 Comments