WASIRA MSAIDIZI WA RAIS SAMIA NDANI YA CCM
#KAZIINAONGEA
Mwanasiasa mkongwe na nguli wa siasa za Tanzania, Stephen Wassira amechaguliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara, jukumu ambalo linampa nafasi ya kuwa msaidizi wa moja kwa moja wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya chama tawala.
Wassira amechaguliwa kushika wadhifa huo kwa kupata kura za ndio asilimia 99.42 ambazo ni sawa na kura 1910 kati ya kura 19 kwa kura 1921.
Mchanganuo wa kura ni kama ifuatavyo:-
Jumla ya wapiga kura ni 1921 Jumla ya kura halali zilizopigwani 1917, kura za hapana zilikuwa saba na za ndio ni 1910 sawa na asilimia 99.42 na kura zilizoharibika ni nne.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments