YAMTAKA MGANGA MKUU KISARAWE KUHAKIKISHA HUDUMA YA AFYA INAPATIKANA ZAHANATI YA BWAMA

 


 YAMTAKA MGANGA MKUU KISARAWE KUHAKIKISHA HUDUMA YA AFYA INAPATIKANA ZAHANATI YA BWAMA

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara, imemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha huduma ya Afya inapatikana wakati wote katika Zahanati ya Bwama Wilayani humo.

Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb), amebainisha hayo wakati anazindua Zahanati ya Bwama iliyopo Wilaya ya Kisarawe hivi karibuni ambapo amesisitiza huduma hiyo ya utoaji wa afya isisimame ili wananchi waweze kupata huduma waliokuwa wanaipata kutoka mbali na kijiji hicho.

Pia Dkt.Jafo amewaasa Wananchi wa Kisarawe kuhakikisha wanawapeleka watoto wao za Sekondari za hosteli ili wakae maeneo ya karibu na shule ili kupata elimu kwa ukaribu kwani Serikali imefanya maendeleo makubwa ya ujenzi wa shule za Sekondari nane pamoja hosteli kwa muda mfupi.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments