Bodi ya Chai Tanzania yajadili uwekezaji wa chai Iringa na Njombe


Bodi ya Chai Tanzania yajadili uwekezaji wa chai Iringa na Njombe

Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya  Diplomasia ya Uchumi inayohasisiwa na Mheshimiwa Dk. Rais Samia Suluhu Hassan, Kaimu Mkurugezi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania (TTB) Bi.Beatrice Banzi amekutana na kuzungumza na Afisa Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania Mh. Nikita Rassokhin kujadili uwekezaji wa chai katika mkoa wa Iringa wilayani kilolo pamoja na Mkoa wa Njombe.

Katika kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya TBT, Jijini Dar es Salaam kilikuwa na mafanikio makubwa hasa kutokana na uwepo wa fursa nyingi za chai kutoka hapa nchini kwenda kuuzwa Urusi.

Katika kuhakikisha biashara ya chai baina ya nchi hizi mbili inaanza TBT imemwalika Mh. Nikita Rassokhin kutembelea mikoa ya Iringa na Njombe mwezi ujao.

Pia akiwa na Maafisa wa TBT atatembelea maeneo yenye Mashamba ya Chai pamoja na Viwanda vinavyochakata, kuchanganya na kufungasha chai.

Anasema," TBT chini ya Wizara ya Kilimo tunaendelea kuyafungua masoko ya chai ya ndani na nje ya nchi, kwa sasa tumeshiriki maonesho kadhaa yanayohusu sekta ya chai na hakika tumeanza kupata masoko ya nje na hii yote ni faida ya diplomasia uchumi chini ya Mh, Rais.Dr Samia Suluhu Hassan na  Waziri wa kilimo Mh. Hussein Bashe."

Post a Comment

0 Comments