Bodi ya Chai Tanzania yashiriki maonyesho ya Gulfood Dubai
Bodi ya Chai Tanzania (TBT) inashiriki katika maonesho makubwa ya chakula ya Gulfood yanayoendelea nchini Dubai (17-21 Februari)
Dhumuni la kushiriki kwenye maonesho hayo ni kufungua masoko, kutafuta wawekezaji kwenye chai na kuchagiza mnada wa Chai wa Dar es salaam. Maonesho hayo yanakutanisha nchi zote duniani kuonesha bidhaa mbalimbali za chakula.
Aidha, Katika nyakati tofauti timu ya Bodi imekutana na kampuni zinazofanya biashara ya kuchanganya chai (Blenders) kutoka nchi mbalimbali, ambapo Chai ya Tanzania imefanyiwa majaribio ya awali na baadhi ya kampuni zilizotembelewa na timu ya Bodi ya Chai na kufanikiwa kupita kwenye majaribio hayo.
Mpaka kufikia tarehe 19/02/2024 kampuni tofauti zimeonesha nia ya kuchukua Wastani wa Kontena 10 za aina tofauti ya Chai kutoka Tanzania. Mazungumzo na wahitaji wa Kontena hizo yanaendelea, ili kufanikisha adhma ya Serikali na Wizara ya Kilimo katika kukuza masoko ya bidhaa za Tanzania kwenye anga za kimataifa na kusaidia kuingiza fedha nyingi zaidi za Kigeni nchini.
Bodi ya Chai inaendelea kuwasihi wadau wote wa Chai nchini Tanzania, kuendelea kusimamia ubora wa Chai wanazozalisha ili kuweza kuhimili ushindani wa masoko ya nje na kupata masoko mengi zaidi.
0 Comments