BODI YA CHAI YATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA BIDHAA ZOTOKANAZO NA CHAI


BODI YA CHAI YATEMBELEA KIWANDA CHA KUZALISHA BIDHAA ZOTOKANAZO NA CHAI

Maafisa wa Bodi ya Chai wametembelea kiwanda cha COSMO kinachohusika kuzalisha bidhaa mbalimbali za urembo wa nywele na ngozi ikiwemo mafuta ya kupaka, sabuni na manukato ya aina mbalimbali. 

Katika ziara hiyo watumishi wa Bodi ya Chai walipata kuona aina mbalimbali za bidhaa za urembo zilizotengenezwa kwa kutumia Chai. Katika mazungumzo na menejimenti ya kiwanda hiko.

Bodi ya Chai imewakaribisha wamiliki wa kiwanda hiko kuja kufanya utafiti wa soko la bidhaa hizo Tanzania na kuweza kujenga kiwanda kitakachotumia malighafi za Chai kwenye bidhaa za urembo zinazotumia Chai.


Aidha, bidhaa nyingi za kiwanda hiko zinatokana na matunda na aina mbalimbali ya bidhaa za kilimo kama vile Sabuni za Parachichi, Kahawa, Papai, Tangawizi na kadhalika. 

Bodi ilieleza kuwa bidhaa hizo zote zinapatikana Tanzania, na tupo tayari kuwaunganisha na mamlaka za Juu kujadiliana namna nzuri ya kufungua kiwanda cha manukato Tanzania na kutumia bidhaa tajwa kama malighafi kiwandani hapo. 


Menejimenti ya Kiwanda hiko ili ahidi kuja Tanzania mwezi Aprili kwa ajili ya kufanya zoezi hilo. 

Hatua hii itawezesha vijana wa Kitanzania kupata ajira zaidi ya 2000 kama kiwanda kitatengenezwa na kupandisha masoko ya bidhaa mbalimbali za kilimo ambazo zitakua zinatumika kama malighafi kiwandani hapo.


Post a Comment

0 Comments