Mama Maria Nyerere: CCM idumishe uwezo wa Taifa kujitegemea
Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere, ameitaka CCM kuendelea kutimiza wajibu wake wa kuzisimamia serikali zake zote mbili ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na uwezo wa kujitegemea, hasa katika kujilisha.
Mama Maria alisema hayo alipokutana na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, aliyefika nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Msasani, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumsabahi na kumjulia hali, leo Alhamisi, tarehe 20 Februari 2025.
“Naomba tu muendelee kusimamia sera ya msingi ya CCM kuhusu kujitegemea… Uhuru wa taifa unakamilika zaidi pale taifa linapojitegemea, hasa katika kujilisha na kuwa na chakula. CCM isiache wajibu wake wa kuzisimamia serikali zake zote mbili ili nchi yetu iendelee kujitegemea,” alisema Mama Maria.
0 Comments