WILAYA YA MTAMA YATATUA MIGOGORO 27



WILAYA YA MTAMA YATATUA MIGOGORO 27

 Mwandishi wetu, Mtama

Migogoro 32 kati ya hiyo 27 imeshatatuliwa kupitia msaada wa kisheria ambayo nikampeni ya Mama Samia kutatua migogoro mbalimbali kwa wananchi ambao hawana uwezo.

Akizungumza na wananchi wa Mnolela leo Februari 21,2025 Mratibu wa Kampeni ya Msaada ya Kisheria ya Mama Samia Wakili Rockus Komba amesema kuwa wamefanya mikutano katika vijiji sita na kuweza kutatua migogoro ikiwemo migogoro ya ardhi pamoja na familia.

Amesema kuwa kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama samia inasaidia sana kwa wananchi ambao hawawezi kuwafikia wanasheria kutokana na kukosekana kwa uwezo wa kifedha.

"Hadi sasa tumeshatatu migogoro 27 kati ya 32 tumeshapatia ufumbuzi ,na iliyobakia tumeshaipeleka sehemu husika ili kupata ufumbuzi naamin hadi tutakapo maliza kampeni hii tutakuwa tumemaliza maeneo migogoro yote ya Halmsahauri ya Mtama."Amesema.Wakili Komba


Naye Mkuu wa dawati la jinsia na watoto Joyce Kitesho alipokuwa anatoa elimu ya unyanyasaji wa kijinsia na migogoro ya ndoa amewataka wanawake wasifumbie macho ukatili wa aina yoyote ambao unaweza kuhatarisha maisha yao

"Wanawake wenzangu nawaomba msifumbie macho maswala ya unyanyasaji majumbani kwetu tutoe taarifa tusifumbie macho"amesema Katesho.

Wananchi wa Mnolela wameishukuru Serikali kwa kuwaletea msaada wa kisheria katika maeneo yao kwani itasaidia sana kuondoa migogoro mingi ambayo inatokea kila wakati kwenye jamii zao.

Zabibu Saidi mkazi wa Mnolela,amesema kuja kwa kampeni ya Mama Samia itasaidia kuondoa changamoto za migogoro katika maeneo yao na kuweza kuleta suluhu katika jamii.

"Kampeni ya msaada wa kisheria utasaidia kwa sisi wananchi wa Lindi kupunguza migogoro ambayo inatokea kila wakati kwenye maeneo yetu, kama hii migogoro ya ndoa nimefurahi sana kuona ipo kwenye orodha kwani wanandoa wengi wananyanyasika majumbani"Amesema Said



Post a Comment

0 Comments