KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YAZINDULIWA LINDI


KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YAZINDULIWA LINDI

Mwandishi wetu, Lindi

Waziri Mkuu Majaliwa Kasimu Majaliwa amewataka wananchi Mkoani Lindi kutumia kampeni ya kitaifa ya msaada wa kisheria ya Mama Samia kutatua changamoto za msaada wa kisheria zinazowakabili. 

Majaliwa ametoa wito huo alipokuwa anazungumza na wananchi Katika uzinduzi wa kampeni hiyo Leo February 19 uliofanyika Katika viwanja vya madini huko Wilayani Ruangwa. 

Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa Amesema Lengo kuu la kampeni hiyo ni kuongeza wigo wa utoaji haki kwa sheria tulizonazo ili wananchi wasio na uwezo waweze kupata haki.

"Wadau mmekuwa na mchango mkubwa sana Huduma hii hapa Lindi imetufikia Rais Samia Suluhu ameguswa na kuanzisha kampeni hii na kuiyachia Wizara ya Katiba na Sheria kuisimamia na kuhakikisha  itapatikana bila gharama yoyote ambapo  mwenye shida  ama matatizo ajiandae kwenda kuhudumiwa na wanasheria wabobevu ambapo hakuna ubaguzi wa rangi dini wala ukabila" amesema Waziri Mkuu  

"Serikali wakati inaanzisha ilipanga kuwafikia wasio na uwezo wakumudu gharama za kisheria wakinamama wenyematatizo msiogope kwenda kwenye vyombo hivyo mkaelezee kero zenu"waziri Mkuu

"Hata Mwanaume ukipigwa gumi usikae kimya dawati lipo kule jeshi la polisi na hata akina mama mkipigwa muende msikae kimya"Amesema waziri Mkuu 


Nae Naibu Waziri Wizara ya Katiba na Sheria Jumanne Sagini amesema mpaka sasa tayari Mikoa 18 imeshatekeleza kampeni hii ambayo uzinduzi ulifanyika mkoani Mwanza na Leo uzinduzi umefanyika katika mkoa wa Lindi.

Nae Lucia Tamba mwakilishi wa watoa msaada wakisheria Mkoa wa Lindi amesema Moja ya migogoro inayo tatuliwa ni ile ya mirathi,wanaume kukataa kuhudumia watoto wao pamoja na ya ardhi.

"Tunaomba tusaidiwe hata pikipiki au baiskeli pia tunaomba chumba kwenye ofisi za serikali kitakachotumika kutolea msaada Tunaomba serikali itutambue wasaidizi wa kisheria kama walivyotambuliwa watoa huduma za Afya kwa ngazi ya kijamii."Lucia Tamba

Mwishoo.

Post a Comment

0 Comments