MIKOA MITATU YAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA AFYA YA UDONGO


MIKOA MITATU YAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI WA AFYA YA UDONGO

Timu ya wataalamu na wabobezi wa kilimo nchini wamekutana Mkoani Arusha kujadili na kupanga namna ya utekelezaji wa zoezi la upimaji afya ya udongo katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro na Manyara.

Watalaamu hao kutoka Wizara ya Kilimo, Sekretariet za Mikoa, Halmashauri za Wilaya, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo (TARI), Taasisi ya Utafiti wa Kahawa (TaCRI), Chuo Kikuu Cha Kilimo Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), Mbeya University of Science and Technology (MUST), Wataalam Wabobezi wa udongo Wastaafu. 


Wamekutana mapema wiki hii mkoani Arusha kujadili na kupanga namna ya utekelezaji wa zoezi la upimaji afya ya udongo katika mikoa mitatu. 

Sambamba na hilo, Wataalamu hao wamefika katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa ya Arusha na Manyara kwa ajili ya kutambulisha zoezi hilo ambalo limelenga kumsaidia mkulima kupanga matumizi ya ardhi ya kilimo zitakazosaidia kuwa na matumizi sahihi ya mbolea na mbinu bora za usimamizi wa ardhi ya kilimo ili aweze kuongeza uzalishaji na tija katika kilimo.


Kuamilika kwa zoezi hili kutasaidia upatikanaji wa taarifa za afya ya udongo katika ngazi ya kata zitakazowawezesha watumiaji mbalimbali wakiwemo;

 Watumiaji hao ambao ni wafanyamaamuzi, watafiti, Maafisa Ugani, wakulima, wafugaji, Wadau wa Maendeleo na watumiaji wengine wa ardhi ya kilimo katika shughuli zao.



Source: Wizara ya Kilimo 

Post a Comment

0 Comments