MRADI WA VIJANA WAZINDULIWA RUANGWA
Mwandishi wetu, Lindi
Mradi wa timiza malengo awamu ya tatu 2024 - 2026 kwa wasichana na wavulana kuanzia miaka 15-24 umezinduliwa Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi ukiwa na lengo la kuwasaidia rika la vijana balehe ambao kwasasa wako katika mazingira hatarishi.
Uzinduzi huo umefanywa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Ummy Nderiananga ambapo amezindua mradi wa timiza malengo awamu ya tatu 2024 - 2026.
Amesema kuwamradi huo una kazi kubwa ya kutoa elimu na hamasa kwa vijana ili kuhakikisha hawaingii kwenye vishawishi vitokanavyo na makundi rika.
"Nawapongeza vijana wote watimiza malengo niliowaona kwenye vibanda kwa kazi nzuri ya kuendelea kufanya hamasa kwa vijana wenzenu na mabinti kuahakikisha hawaingii kwenye vishawishi kwakua maambukizi ya virusi vya UKIMWI bado ni changamoto hasa kwa miongoni mwa rika la vijana balehe wenye miaka 15 -24" amesema Nderiananga
Unajua Ukimwi na virusi vya ukimwi ni tatizo linalochangia kutokua na maendeleo kwakua ukimwi unachangia kupungua kwa pato la taifa, kushuka kwa kiwango cha kufanya kazi, kuongezeka kwa yatima na kuongezeka kwa vifo na kupungua kwa mda wa kuishi"
"Nitoe wito kwa wadau wote kuweka mkazo katika kujikinga na VVU na kutumia dawa kwa usahihi kwa walio na maambukizi na kuwawezesha kiuchumi Ili waweze kutoa mchango katika kuongeza maendeleo ya nchi" amesema Nderiananga
Pia Amesema hadi kufikia sasa asilimia 90% wanajua hali zao na kumekuwa na kupungua kwa unyanyapaa kwa walio athirika na hamasa kwa waathirika wasiache kutumia dawa.na kuongeza hamasa kwa wanaume kujitokeza kupima Afya zao.
Catherine Joachim Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania amesema tume ya kudhibiti UKIMWI Tanzania imeweka mikakati na malengo ya kudhibiti ugonjwa huo ifikapo 2030.
Amesema takribani watu 60,000 wanapata maambukizi mapya ya kila mwaka ikilinganishwa na watu 72,000 kwa mwaka 2015 - 2016 ambapo mpango wa kitaifavwa kudhibiti ukimwi uliweka malengo ya kufikisha maambukizi mapya 15,000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2026.
"Maambukizi kwa wanawake ni makubwa ambapo 5.6% wanapata maambukizi tukilingania na wanaume wanambaambukizi mapya 3% na vijana wenye umri kuanzia Miaka 15 - 24 wamekua wakichangia ongezeko la maambukizi kwa takribani theluthi Moja kwa mwaka na maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto yameongezeka kwa asilimia 8.4 tukilinganisha na lengo la kufikia 5%.
Nae Naibu Waziri wa Afya Dr Godwin Molel Amesema Rais Samia Suluhu Hassan mwaka Jana alitakiwa kwenda kwenye kikao cha umoja wa mataifa lakini mbunge wa Ruangwa Kasimu Majaliwa alimuwakilisha ambapo kwenye masuala ya afya tepiga hatua sana.
Hata ukiangalia kipindi Cha nyuma mgonjwa alikuwa akipata uvimbe chini ya sakafu ya ubongo alikua anapasuliwa kichwa unakaza takribani mwaka mzima na unapoteza kumbukumbu mwaka mzima ila kwa sasa kichwa hakipasuliwi tena inachukuliwa mashine kidogo inapitishwa puani unatolewa uvimbe unarudi nyumbani bila kupoteza kumbukumbu haya ni maendeleo makubwa.
0 Comments