NSEKELA AWATAKA WATUMISHI BODI YA CHAI KUFANYAKAZI KWA USHIRIKIANO
Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Chai (TBT), Bw. Abdulmajid Nsekela amewataka wafanyakazi wa Bodi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na bidii katika kuiendeleza tasnia ya chai nchini.
Bw. Nsekela ametoa rai hiyo kwenye hotuba yake wakati akizungumza katika kikao cha Menejimenti kilichofanyika Makao Makuu ya TBT ambapo pia alikadhiwa rasmi ofisi na Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Bw. Umande.
Bw. Nsekela amesema, tasnia ya chai inaweza kuwa na mchango mkubwa zaidi hasa kama mnyororo mzima wa thamani katika tasnia hiyo ukitumiwa vema.
"Katika kuhakikisha sekta hii inakuwa zaidi na kuendelea kuchangia pato la taifa ni lazima kuwe na jitihada za ndani ambapo hapa ni watendaji wenyewe wa bodi na katika hilo naona kazi mnafanya nzuri hivyo tuendelee kubuni na kuiendeleza sekta" amesema Nsekela.
Ameongeza,"Binafsi niwaahidi kuendelea kutoa ushirikiano mkubwa zaidi katika kuiendeleza sekta ìli mwisho wa siku chai nyingi iweze kuwa inalimwa, inavunwa, inakuwa processed na kisha kupelekwa nchi ya nchi as final product."
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBT, Bi. Beatrice Banzi amemhakikishia Bw.Nsekela ushirikiano huku akizitaka kampuni zinazofanya kazi katika tasnia ya chai kushiriki kikamilifu katika kutimiza maono ya Mwenyekiti mpya na Bodi kwa ujumla.
#chaiyetufahariyetu
0 Comments