RAIS SAMIA NA KIPAUMBELE CHA SEKTA YA AFYA


RAIS SAMIA NA KIPAUMBELE CHA SEKTA YA AFYA  

*●Aagiza ukarabati wa Hospitali ya Wilaya ya Korogwe*  

*#KAZIINAONGEA*

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi hodari, shupavu na mpenda maendeleo, kama inavyojidhihirisha katika ziara zake mbalimbali ikiwemo ziara inayoendelea mkoani Tanga.

Katika ufuatiliaji  utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini ikiwemo ya afya, Rais Samia amemuagiza Waziri wa Afya Jenista Mhagama kutoa fedha kwa ajili ya kukarabati Hospitali ya Wilaya ya Korogwe (Magunga) ili wananchi wapate huduma bora za afya.

Ametoa maagizo hayo Februari 24, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Korogwe chuo cha ualimu, katika ziara yake mkoani Tanga yenye lengo la kuzindua na kukagua miradi mbalimbali iliyotolewa fedha na Serikali. 


"Changamoto nyingine iliyotajwa hapa ya ukarabati wa hospitali, na vizuri niko na Waziri wa Afya Jenista Mhagama, juzi tu tulikuwa na mgeni, katika maongezi yetu kuna visenti tumevipata, naomba vimege ulete kwenye hospitali hii Ili vije kufanya ukarabati," ameagiza Rais  Samia.

*#AZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments