SAMIA BOND YAORODHESHWA DSE
*#KAZIINAONGEA*
Samia Infastructure Bond hati fungani Mahususi inayotolewa na Benki ya CRDB, kwa ajili ya kufadhili miradi muhimu ya miundombinu nchini Tanzania, hasa ujenzi wa barabara chini ya Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA), imeorodheshwa kwenye soko la hisa la Dar es Salaam, hatua hiyo imejiri baada ya kukusanywa kiasi cha bilioni 323 kutoka Taasisi mbalimbali na wawekezaji binafsi.
Zoezi hilo limeongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa kwa kupiga kengele ikiwa ni ishara ya kuorodhesha Samia Infastructure Bond kwenye soko la hisa la Dar es Salaam.
Samia Infastructure Bond inatazamiwa kutatua changamoto ya upatikanaji wa fedha kwa ajili ya malipo ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara hivyo kuharakisha maendeleo ya miundombinu muhimu kwa usafirishaji wa abiria, mizigo na huduma na bidhaa.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments