SERIKALI YADHAMIRIA KUIMARISHA USALAMA MTANDAONI
#KAZIINAONGEA
Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeonesha dhamira thabiti katika kuimarisha usalama wa mtandaoni kwa kuzindua kampeni ya elimu kwa umma kuhusu utapeli wa mtandaoni iitwayo "SITAPELIKI".
Kampeni hii inayosimamiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kwa kushirikiana na watoa huduma wa makampuni ya simu za mkononi, inalenga kuwaelimisha wananchi juu ya mbinu za kujilinda dhidi ya matapeli wa mtandaoni.
Uzinduzi wa kampeni hii umefanyika jijini Arusha na unatarajiwa kuwa na matokeo chanya kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano nchini.
Hii ni hatua nzuri kwa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kuchukua hatua madhubuti katika kulinda wananchi dhidi ya uhalifu wa mtandaoni. Na kuhakikisha teknolojia ya mawasiliano inabaki kuwa salama na yenye manufaa kwa jamii yote.
*#KAZIINAONGEA*
0 Comments