SERIKALI YAJENGA MAJENGO YA KISASA HOSPITALI YA WILAYA NKASI


SERIKALI YAJENGA MAJENGO YA KISASA HOSPITALI YA WILAYA NKASI

#KAZIINAONGEA

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imejenga majengo zaidi ya matano katika Hospitali ya Wilaya ya Nkasi, iliyopo Namanyere, Mkoa wa Rukwa.

Majengo hayo yanayotoa huduma muhimu za afya kwa wananchi yakiwemo ya huduma za dharura.

Haya ni kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wanaohitaji matibabu ya haraka.

Jengo la Utawala, ni maalum kwa  shughuli za kiutawala za hospitali hiyo.

Wodi za Wanaume, Wanawake, na kulaza na kutibu wagonjwa wa makundi mbalimbali.

Jengo la Upasuaji hili ni jengo la kisasa lenye  vyumba vya upasuaji vilivyo na vifaa vya kisasa kwa ajili ya upasuaji mkubwa na mdogo.

Maabara kwa ajili ya kufanya vipimo mbalimbali vya uchunguzi wa magonjwa.

Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto kinachotoa huduma za uzazi salama, kliniki za wajawazito, na huduma za watoto wachanga.

Kitengo cha uangalizi maalum kwa Watoto Wachanga (NCU), hiki  kimeanzishwa kwa ajili ya kuhudumia watoto wachanga wenye mahitaji maalum ya kiafya.

Jengo la Dawa na Vifaa Tiba ni kwa ajili ya kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa.

Majengo haya yamejengwa kwa viwango vya kisasa ili kuhakikisha kunakuwa na utoaji wa haraka na bora wa huduma za afya kwa wakazi wa Wilaya ya Nkasi na maeneo jirani.

#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments