TANZANIA, IRELAND ZASHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA AFYA


TANZANIA, IRELAND ZASHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA AFYA

#KAZIINAONGEA

 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Ireland zimesaini hati ya makubaliano katika Sekta ya Afya ya kuendeleza ushirikiano uliopo ikiwemo kubadilishana uzoefu baina ya watalaam katika nchi hizo mbili, kufanya utafiti wa matibabu pamoja na kusaidia katika hatua za lishe kwa kupunguza udumavu wa watoto. 

Makubaliano hayo yamesainiwa Februari 19, 2025 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe na Mkurugenzi wa Shirika la 'Wellbeing and Global Health' la nchini Ireland, Dkt. Philip Crowley na kushuhuhudiwa na Waziri wa Afya Jenista Mhagama pamoja na Balozi wa Ireland nchini Tanzania Nicola Brennan. 

"Napenda kuishukuru Serikali ya Ireland kwa kuwa mshirika muhimu katika uboreshaji wa huduma za afya nchini Tanzania, Serikali yetu chini Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, itaendelea kushirikiana na watendaji wa Ireland na watendaji wa huduma za afya katika kuboresha Sekta ya Afya kwa ustawi wa wananchi wa Tanzania," amesema Dkt. Shekalaghe.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments