TANZANIA YAPANGA MIKAKATI YA KULITUMIA IPAVYO SOKO LA KOROSHO LA NCHI ZA GHUBA KUPITIA UAE


TANZANIA YAPANGA MIKAKATI YA KULITUMIA IPAVYO SOKO LA KOROSHO LA NCHI ZA GHUBA KUPITIA UAE

Ubalozi wa Tanzania UAE kwa kushirikiana na Bodi ya Korosho Tanzania yapanga mikakati ya kulitumia ipasavyo soko la Korosho la Nchi za Ghuba kupitia Dubai, UAE ambapo ndio kitovu cha biashara katika ukanda huo.

Hayo yamebainshwa wakati wa kikao kati ya Ubalozi na Ujumbe wa Tanzania uliotembelea Ubalozi tarehe 24 Februari, 2025 katika kikao maalum cha kupanga mkakati huo.


Itakumbukwa kuwa, ujumbe wa Tanzania uluobeba wajumbe 15 ulishiriki Mkutano wa Dunia wa Korosho uliofanyika katika Hoteli ya Hilton Habtoor City Dubai kuanzia tarehe 21 hadi 23 Februari 2025. 

Ujumbe huu uliongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania Bw. Francis Alfred.
Katika Mkutano huo wa Dunia, Korosho ya Tanzania ilisifiwa kuwa ni miongoni mwa korosho bora duniani kutokana na vigezo vya korosho vya soko la kimataifa duniani vikiwemo rangi nyeupe, ukubwa wake na ladha nzuri. Tanzania ni nchi ya pili Afika kuzalisha Korosho na ni nchi ya tano Duniani.


Aidha, katika kikao na Ubalozi ilikubalika kushirikiana kutafuta wawekezaji kwenye viwanda vya kubangua korosho ili kuongeza thamani ya korosho zilizochakatwa na kuuzwa nje kwa kuwa hadi sasa 80% ya korosho zinazouzwa nje ni ghafi. Kikao kilifahamisha kuwa lengo la Serikali ifikapo mwaka 2030 100% ya korosho inayozalishwa yote ibanguliwe nchini Tanzania. 

Aidha, ilifahamishwa kuwa tayari Serikali imetenga eneo la kongani ya viwanda inayojengwa kijiji cha Maranje Halmashauri ya Mji Nanyamba mkoani Mtwara. Kongani hilo lina jumla ya hekari 1,572 linatarajiwa kuwa na viwanda zaidi ya 60 ambapo litagharimu takribani Sh bilioni 5.6 hadi kukamilika kwa mchakato mzima wa ujenzi. 


Kwa muktadha huo, Balozi za Tanzania zinahamasishwa kutafuta wawekezaji wa Viwanda vya kuchakata korosho ili kuweza kunufaika ipasavyo na zao hilo.

Kongani hiyo inakwenda kuongeza ajira 35,000 za moja kwa moja, uuzaji wa korosho na bidhaa zake badala ya kuuza tu korosho ghafi kama vile ganda lenyewe.
@wizara_ya_kilimo @wizara_mambo_ya_nje_tz

Source: @tzembassyinuae

Post a Comment

0 Comments