USHINDANI KUSHUSHA BEI YA DAWA, VIFAA TIBA, KUIMARISHA MFUKO WA BIMA YA AFYA


USHINDANI KUSHUSHA BEI YA DAWA, VIFAA TIBA, KUIMARISHA MFUKO WA BIMA YA AFYA

#KAZIINAONGEA

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, Februari 18, 2025, amefanya majadiliano na Bodi ya Ushauri pamoja na Menejimenti ya Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) kuhusu mikakati bora ya kukabiliana na bei kubwa za dawa nchini. 

Katika majadiliano hayo, Dkt. Mollel ameainisha changamoto ya kuwepo kwa hali ya soko ambalo linadhibitiwa na watu wachache (monopoly), hali inayosababisha bei za dawa kuwa kubwa na kuongeza gharama za tiba kwa wananchi.

Dkt. Mollel amebainisha kuwa, kwa kuanzisha ushindani katika soko la dawa na vifaa tiba, bei hizo zitaweza kushuka, na hivyo kuboresha upatikanaji wa huduma za afya. 

Ameongeza kuwa, mpango huo utasaidia kuimarisha Mfuko wa Bima ya Afya kwa Wote, na kuongeza upatikanaji wa huduma bora kwa wananchi.

*#KAZIINAONGEA*

Post a Comment

0 Comments