WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO MBINGA WAKABISHIWA VITAMBULISHO
Jumla ya wafanyabishara ndogondogo 70 kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga wamekabidhiwa vitambulisho na Katibu Tawala Wilaya ya Mbinga Bi. Pendo Ndumbaro tarehe 24 Februari 2025.
Moja ya faida ya vitambulisho hivyo ni kuwawezesha wafanyabiashara hao kutambulika katika mamlaka mbalimbali hususan Mamlaka ya mapato Tanzania pamoja taasisi za kifedha.
Aidha ni fursa mojawapo kwa Halmashauri katika kujua idadi ya wafanyabiashara ndogondogo katika maeneo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga katika kuendeleza / kuboresha miundombinu rafiki ya kibiashara.
0 Comments