WAZIRI MKUU ASHUHUDIA MATREKTA YAKIKABIDHIWA RUANGWA


WAZIRI MKUU ASHUHUDIA MATREKTA YAKIKABIDHIWA RUANGWA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) akishuhudia makabidhiano ya matrekta kati ya Wizara ya Kilimo na Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa tarehe 22 Februari 2025. 

Makabidhiano hayo yamefanyika baina ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Frank Chonya na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Dkt. Hussein Mohamed Omar (anayesimamia Usalama wa Chakula na Maendeleo ya Mazao). 

Wilaya ya Ruangwa imepokea matrekta matano ikiwa ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kukabidhi zana za kilimo kwenye vituo 45 vya kutolea huduma nchini.

Post a Comment

0 Comments